Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Kamwe usidharau nguvu za wapinzani wako katika jambo lolote lile,kwani huwezi tambua uwezo wao dhidi yako

Kamwe usidharau nguvu za wapinzani wako katika jambo lolote lile,kwani huwezi tambua uwezo wao dhidi yako

Written By Unknown on Wednesday, 16 October 2013 | Wednesday, October 16, 2013




Siku moja Sungura alijidai na kujisifia jinsi ambavyo anaweza kukimbia haraka, na pia akawa akimcheka Kobe jinsi alivyo taratibu katika mambo yake na kumwita kilaza.
Lakini baada ya kushindana kukimbia Sungura alishangazwa kuona jinsi ambavyo kobe alimshinda katika zile mbio, Sungura alikubali ushindi na kuona ilikuwa ni utani tu kwake.
Shindano lililofuata, Mbwa mwitu alikuwa ndiye refa wa shindano. Baada ya mbio kuanza Sungura alianza kwa spidi na kumshinda Kobe kama kila mtu alivyofikiri.
Sungura alikimbia mpaka anafika katikati bila kumwona Kobe sehemu yoyote ile. Sungura akiwa anajisikia joto kali mwilini na kachoka akaamua apumzike kidogo kwani hata Kobe angempita bado sungura alikuwa na uwezo wa kuwahi kumaliza mbio na kuibuka mshindi.
Wakati huo Kobe alikuwa akitembea taratibu tena kwa step akimfuata sungura bila kukoma hata kama alichoka vipi yeye aliendelea kwenda.
Sungura kutokana na lile joto na uchovu na baada ya kupata kaupepo mwanana pale alipopumzika, basi akapitiwa na usingizi mzito na kulala kwa muda, aliposhtuka toka usingizini bila kumwona Kobe, akatimua mbio ili akamalizie mbio na kuibuka mshindi.
Ile anafika mwisho akashangaa kumwona kobe kashatangazwa mshindi, Sungura alizimia kwa hasira.
Funzo
Kamwe usidharau nguvu za wapinzani wako katika jambo lolote lile,kwani huwezi tambua uwezo wao dhidi yako
Kama ina maana kwako ruksa kushare
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi