Mtuhumiwa wa ugaidi AL Sanusi Al Libi |
Akionekana mwenye kujiamini, Anas al-Libi alimwambia jaji
anayesikiliza kesi hiyo kwenye mahakama ya mjini New York, kuwa hana
hatia dhidi ya tuhuma za kuhusika na tukio la ulipuaji wa balozi za
Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.
Anas al-Libi amesomewa zaidi ya mashtaka sita ikiwemo kupanga njama za mauaji, utekaji nyara, mauaji ya halaiki pamoja na uharibifu wa mali na majengo ya usalama ya Marekani, mashtaka ambayo yote amekana kuhusika nayo.
Hata hivyo hatua ya serikali kumfikisha mtuhumiwa huyo wa ugaidi kwenye mahakama ya kiraia mjini New York imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi ambao wanataka mtuhumiwa huyo ashtakiwe kwenye mahakama ya gereza la Guantanamo kutokana na makosa aliyotenda.
Anas al-Libi alikamatwa na makomandoo wa Marekani kwenye viunga vya mji wa Tripoli nchini Libya octiber 5 mwaka huu na kusafirishwa hadi mjini New york ambako alifunguliwa kesi mwaka 2000.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!