MACHO ya Dunia ya wapenda soka yalitua kwa Gareth Bale siku aliyotambulishwa pale Real Madrid. Uhamisho wake wa kutoka Tottenham Hotspur umemfanya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa, alipohamishwa kwa Pauni 85 milioni. Hilo ndilo lililowafanya mashabiki kusubiria kwa hamu utambulisho wake.
Bale, aliyekuwa ameandamana na familia yake
ikiwamo mchumba wake, mrembo Emma Rhys Jones alijiandaa kwa tukio hilo
ikiwamo kunyoa nywele zake vizuri. Bale anaripotiwa kutumia Pauni sita
(Sh15,000) kunyoa nywele zake siku hiyo kabla ya kwenda Santiago
Bernabeu kutambulishwa.
Wahispaniola walipagawa baada ya kuona mtindo wa
nywele alionyoa Bale, wakakimbilia saluni kutaka na wao wanyolewe kama
alivyonyoa Bale. Hawakujali ilimgharimu kiasi gani Bale kutengeneza
mwonekano huo wa nywele zake.
Si suala la gharama iliyotumika kwenye kunyoa.
Bale hawezi kuingia kwa mastaa kama Jennifer Lopez, Jennifer Aniston,
Rihanna, Michael Douglas, David Beckham, ambao wameingia kwenye rekodi
ya kuwa watu walionyoa nywele zao kwa gharama kubwa zaidi.
Rihanna aliwahi kuny’oa nywele zake kwa Dola
2,000, wakati Beckham anaripotiwa kuwahi kutumia Dola 6,000 kwa ajili ya
kunyoa tu. Lakini, unafahamu ni nani aliyemnyoa Bale?
Klabu mahasimu wa Ligi Kuu, Manchester United na
Manchester City nyota wake wanaweza kupishana kwenye mambo mengi, lakini
hilo haliwezi kuwa kwa kinyozi huyu. Hapo, wote wanazungumza lugha moja
na kuweka uhasama wao kando. Unajua kwa nini?
Kinyozi huyo, Daniel Johnson, ndiye anayewapamba
kwa mikato ya mitindo tofauti ya nywele zao. Kunyoa mastaa kumemfanya
kuwa mtu maarufu sana England kwa sasa.
Mastaa wote unaowatamani kuwagusa japo unywele tu
au kujaribu kuiga mitindo yao ya nywele, wananyoa kwa kinyozi Daniel.
Kinyozi Daniel amekuwa maarufu kwa sababu ananyoa mastaa na watu
mashuhuri wanaotamba kwenye muziki, soka, filamu na tasnia nyingine za
uburudishaji.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!