WASANII wa Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi waliofika kuzuru kaburi la aliyekuwa legendary wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, wameibua simanzi upya na kumsababisha mama wa marehemu, Flora Mtegoa kuangua kilio upya kwa mara nyingine.
Tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi lilitokea Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii hao walifika kutoa heshima zao baada ya kushindwa kufika tangu nguli huyo alipofariki dunia Aprili 7, mwaka jana.
BAADHI YA WASANII MBALIMBALI WA AFRICA MASHARIKI WAKIWA KATIKA KABURI LA KANUMBA |
BATULI AKILIA |
“Mwanangu pumzika kwa amani huko uliko, mama yako bado nina maumivu,” alisikika mama Kanumba huku akiangua kilio kwa uchungu.
Wakati mama Kanumba akiendelea kulia, baadhi ya wasanii wa Bongo, Haji Adam ‘Baba Haji’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na Hashim Kambi ‘Wingo’ walilazimika kumbembeleza mama huyo huku nao wakilia.
Mbali na kuzuru kaburi la marehemu Kanumba wasanii hao kutoka nje ya Bongo, Sinia (Rwanda), Joy Liz (Kenya), Okuyu (Uganda) na wengineo, walitinga kurekodi filamu ya Wekeza Inalipa kisha kurejea nchini kwao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!