MIAKA tisa imepita tangu kipaji cha uimbaji cha mwanamuziki Sarah Kaisi ‘Shaa’ kilipoibuliwa katika mashindano ya Coca Cola Pop Star akiwa na Witness Mwaijaga na Langa Kileo (marehemu). Mwanamuziki huyo anasema alipoanza kuwika katika muziki, alijiwekea malengo, moja kati ya hayo ilikuwa ni kuanzisha familia. Yafuatayo ni mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni.
Ismailniyonkuru.info: ‘Ni mipango gani ulijiwekea mara baada ya jina lako kuanza kuwika katika Bongo flava?
Shaa: Mikakati yangu ilikuwa ni
kufanya muziki kwa kipindi cha miaka saba ndipo nianzishe familia ambayo
itakuwa na watoto wawili. Lakini sasa imefika miaka tisa ndoto
haijatimia. Kuna sababu mbalimbali ambazo bado nazifanyia kazi.
Nilipanga nikishazaa niwaangalie kwa karibu watoto
kwa malezi huku nikiendelea na kazi yangu ya muziki. Sikuhitaji kupata
watoto mapema, mimi kama Shaa naamini kuwa mtoto anakuja kwa kupanga,
siwezi kuzaa watoto mapema kisha nikawalaza njaa.
Ismailniyonkuru.info: Ni kitu gani kinakukwamisha katika kuanzisha familia, hujampata mtarajiwa?
Shaa: Kiukweli mtarajiwa wangu siwezi kumwanika kwani kwa sasa jina lake bado ni siri yangu, mtamjua tu mambo mazuri hayataki haraka.
Mwanaspoti lilitaka kujua mengi kutoka kwa
mwanamuziki huyu anayetamba na wimbo wa ‘Lavalava’ hasa baada ya kuwapo
tetesi kwamba amejiunga na sehemu ya Kundi la Wanaume Family yaani
kituo cha Mkubwa na Wanawe kilicho chini ya Said Fella.
Ismailniyonkuru.info: Shaa, kuna tetesi kwamba sasa umejiunga katika moja ya matawi ya Wanaume Family, kuna ukweli wowote katika hili?
Shaa: Mimi ni msanii katika lebo
ya MJ Records kwa kipindi cha miaka minne sasa. Lakini hivi karibuni
nimekuwa nikisimamiwa na mameneja mbalimbali wakiwamo AY na baadaye
nilianza kusimamiwa na Babu Tale.
Nimekuwa kwa Tale kwa kipindi kirefu sasa lakini
yeye akaona si mbaya kama akimwingiza Fella naye ili kuukuza zaidi
muziki wangu.
Ismailniyonkuru.info: Katika Kundi la TMK umesaini mkataba wa aina gani?
Shaa: Mkataba wangu ni wa miezi
sita tu. Nikiwa TMK nitakuwa nikiwafundisha muziki vijana wa kituo cha
Mkubwa na Wanawe na nitafanya nao kazi angalau mbili za muziki. Mfano
sasa nimesharekodi kazi inayoitwa ‘Sugua Gaga’, kazi hii nimefanya na
watoto wa kituo cha Mkubwa na Wanawe na inatarajiwa kuachiwa katika
vituo mbalimbali vya redio wiki ijayo, huku video ya wimbo huo ikiwa
inapikwa jikoni.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!