Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BAADA YA TERENCE SINTUNGURUZA KUJIUZULU HUYU HAPA ASHIKA WAZIFA WAKE

BAADA YA TERENCE SINTUNGURUZA KUJIUZULU HUYU HAPA ASHIKA WAZIFA WAKE

Written By Unknown on Thursday, 17 October 2013 | Thursday, October 17, 2013


Bernard Busokoza
Nchini Burundi, Bwana Bernard Busokoza wa kabila wa watutsi na anayetoka chama cha Uprona, ameteuliwa kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi .
Bernard Busokoza mwenye umri wa miaka 60 , anachukua nafasi ya Terence Sinunguruza aliyejiuzulu hivi karibuni baada ya kupoteza imani ya chama chake cha Uprona kwa madai kwamba alipuuza maslahi ya chama na kujiendeleza yeye binafsi.
Terence Sinunguruza
Busokoza alikuwa afisaa wa zamani wa jeshi la zamani la Burundi baada ya kupata elimu ya kijeshi nchini Ugiriki. Hata hivyo alijihusisha na maswala ya biashara hasa katika sekta ya mawasiliano baada ya kustaafu kutoka katika jeshi.
Anamiliki mojawapo ya kampuni kubwa ya mawasiliano nchini humu.
Uteuzi huo wa Bernard Busokoza umeidhinishwa Jumatano jioni na bunge pamoja na baraza la seneti.
Hata hivyo kulikuwa na pingamizi kuhusu uteuzi wake hasa kutoka kwa wabunge wa chama cha (CNDDFDD) cha Rais Pierre Nkurunzinza wakisema kuwa aliwahi kuhusika na mapinduzi ya kijeshi yaliyosababisha kifo cha rais wa kwanza wa kihutu Milkior Ndadai
Makamu wa rais aliyemtangulia, Terence Sinunguruza alijiuzulu kutokana na shinikizo za wanachama wenzake wa (UPRONA) waliodai kuwa haonekani kutetea masilahi ya chama chake.
Chama hicho kilimtaka Rais Pierre Nkurunziza kumfuta kazi Sinunguruza, aliyetuhumiwa kwa kusababisha migawanyiko chamani tangu kuchukua wadhifa huo miaka mitatu iliyopita.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi