wakaguzi wa OIAC |
Shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya silaha za kemikali kwenye vita OPCW ambalo juma lililopita lilipewa tuzo la Nobel, limesema kuwa waangalizi wake wanapewa ushirikiano wa kutosha na utawala wa rais Bashar al-Assad licha ya wanajeshi wao kutokuwa na umiliki kwenye baadhi ya maeneo.
Kauli hii ya shirika la OPCW inatolewa wakati huu kukiwa na hofu ya waangalizi hao kuweza kufika kwenye ngome zinazoshikiliwa na wapiganaji wa jeshi huru la Syria kutokana na kukosa hakikisho la usalama ingawa wanaamini watamaliza zoezi lao ndani ya muda.
Wakaguzi hao wamesema Octoba 12, shambulio la kujitowa muhanga limetokea karibu na Hoteli Damas, eneo wanakoeshi wakaguzi hao, makombora pia yamerushwa juma hili. Tume hiyo ya wakaguzi ipo nchini Syria tangu Octoba Mosi na ianundwa na zaidi ya watu sitini.
Asilimia kubwa ya zana hizo za kemikali zimekaguliwa na wakaguzi hao wa OPCW. Licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa la Usalama, shirika hilo litatekeleza jukumu lake kwa wakati kama ilivyo pangwa katika kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha Septemba Mosi mwaka 2013
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!