MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund Robert Lewandowski atakunja kitita cha paundi milioni 10 wakati atakapojiunga na Bayern Munich kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu huu.
Mabosi
wa Bayern wamepuuza taarifa kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Poland
ameamua kubadili mawazo kujiunga na klabu hiyo na kusisitiza kuwa uvumi
huo utakwisha wakati watakapofanya usajili wa awali katika kipindi cha
dirisha dogo la usajili Januari mwakani.
Katika
kipindi hiki haruhusiwi kufanya mazungumzo yoyote rasmi kuhusiana na
uhamisho huo mpaka Januari lakini kumekuwa na tetesi kuwa Bayern
wamepanga kumpa mkataba mnono wa miaka minne ambao utamuwezesha kuwa
analipwa kiasi cha paundi 150,000 kwa wiki. Taarifa
zozote rasmi za Bayern kumnyakuwa nyota huyo zitakuwa ni pigo kwa
vilabu vya Manchester United na Chelsea ambao nao wamekuwa wakimtolea
macho kwa kutaka kumsajili.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!