Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WAFANYAKAZI WARUDI KAZINI BAADA YA BUNGE LA MAREKANI KUFIKIA MAKUBALIANO YA KUIWEZESHA SERIKALI KUKOPA

WAFANYAKAZI WARUDI KAZINI BAADA YA BUNGE LA MAREKANI KUFIKIA MAKUBALIANO YA KUIWEZESHA SERIKALI KUKOPA

Written By Unknown on Friday, 18 October 2013 | Friday, October 18, 2013

Maelfu ya wafanyakazi nchini Marekani wameanza kurejea kwenye vituo vyao vya kazi saa chache baada ya wabunge wa Republicans na wale wa Democrats kufikia makubaliano kuhusu kuiwezesha Serikali kukopa ili kuendesha shughuli zake zilizokuwa zimesimama.

Makubaliano yaliyofkiwa hapo jana yataiwezesha serikali ya Marekani kujiendesha hadi mwezi january mwakani kabla ya wabunge hao kurejea tena kwenye meza ya mazungumzo kusaka suluhu ya kumaliza kabisa tofauti zao.
Rais Barack Obama tayari ametia saini muswada uliowasilishwa na wabunge hao na kupongeza hatua iliyofikiwa huku akitoa wito wa jambo hili kumalizwa ili kutorejea tena kwenye hali hii.
Kwa upande wake seneta wa republican kwenye jimbo la Arizona, John McCain anasema kuwa amepigana vita kupinga mpango wa afya wa Obama na ataendelea kufanya hivyo kwenye siku zijazo licha ya sasa suala hilo kufikiwa muafaka.
Chama cha rais Obama kina muda wa miezi mitatu ya kujadili na kupata ufumbuzi wa muda mrefu. Lengo hasa ikiwa kuhakikisha kimewaweka chini wafuasi wa  Republican kabla ya uchaguzi wa bunge mwaka ujao, ili kurejesha uwengi katika baraza la bunge na seneti, na hivo kumruhusu rais Obama kumaliza muda wake wa pili na kutekeleza baadhi ya ahadi zake, bila kutiwa vikwazo na Baraza la Wawakilishi ambao waonekana kila wakati kumtilia ngumu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi