NAIBU wa Rais William Ruto, anatarajiwa
kurudi nchini kutoka The Hague, mwishoni mwa wiki kwa sababu Rais Uhuru
Kenyatta, ataondoka kwenda Addis Ababa kuhudhuria kikao maalumu cha
Muungano wa Afrika.
Bw Ruto ataondoka The Hague, Uholazi baada ya kesi inayomkabili kuahirishwa wikendi.
Kesi ya Bw
Ruto na aliyekuwa mtangazaji Bw Joshua Sang, imepangwa kuendelea hadi
Novemba 1, ili kupisha inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta Novemba 12.
Hata hivyo, mahakama haijaamua ikiwa kutakuwa na kikao kingine mwaka huu kama upande wa mashtaka ulivyoomba.
Hapo
Alhamisi, mawakili wa Bw Ruto waliendelea kumhoji shahidi wa pili
nambari 326, ingawa sehemu kubwa ya kikao hicho iliandaliwa faraghani.
Baadaye mawakili wa Bw Sang watamhoji shahidi huyo. Upande wa mashtaka
pia utamhoji kabla ya kukamilisha ushahidi wake. Rais Kenyatta
amenukuliwa akisema kwamba kikatiba, hafai kuwa nje ya nchi wakati mmoja
na naibu wake, madai aliyotumia alipokosa kuhudhuria kikao cha Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Rais Kenyatta
pia alikosa kuhudhuria kikao jijini Brussels September 16 kuhusu hali
ya usalama katika upembe wa Afrika, kutokana na mzozo wa Somalia kwa
sababu Bw Ruto alikuwa The Haque.
Rafiki wa korti
Wakati huo
huo, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilikataa ombi la raia wa
Kenya Bi Moraa Gesicho aliyetaka kushirikishwa katika kesi dhidi ya
Rais Kenyatta kama rafiki wa korti.
Mahakama hiyo
ilisema Bi Gesicho hana ujuzi wa kuchaganua ripoti ya Tume ya Uchunguzi
wa Ghasia za baada ya Uchaguzi (CIPEV), inayofahamika kama ripoti ya
Waki. “Fauka ya hayo, mahakama hii haidhani kwamba kushirikishwa kwake
kutakuwa na manufaa katika kuchaganua ripoti hiyo. Kwa msingi huu,
mahakama hii haidhani kwamba uchaganuzi unaokusudiwa utahitajika katika
kuamua kesi hii,” majaji Kuniko Ozaki, Robert Fremr na Chile Eboe-Osuji
walisema kwenye uamuzi wao.
Bi Gesicho
aliwasilisha ombi lake Septemba 9 akitaka ashirikishwe kama rafiki wa
mahakama akisema alikuwa tayari kujitolea kufanya utafiti kuhusu ripoti
ya Waki, ikiwa mahakama ilihitaji ripoti hiyo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!