BAADHI ya wabunge wametaja hatua ya aliyekuwa mpatanishi mkuu nchini Kofi Annan ya kuitetea Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kama 'isiyofaa’ na kumkashifu kwa kuja nchini mmamo 2008 kuendeleza ajenda ya mahakama hiyo, iliyobuniwa chini ya Mkataba wa Roma.
Wabunge hao
walisisitiza kauli za viongozi wengi wa Kiafrika kuwa ICC inalenga
kuyaadhibu mataifa ya Kiafrika, kwani haijawashtaki wachochezi wa ghasia
katika nchi nyingine, ambako maelfu ya watu wameuawa
“Huu ni
utaratibu mbaya na tunapaswa kujiuliza maswali kadha; kama ni kuhusiana
na rangi ya ngozi zetu, utofauti katika jamii zetu, ni kigezo gani
ambacho ICC hutumia kuorodhesha makosa kama uhalifu dhidi ya ubinadamu,
na inayopaswa kuyaacha,” akasema Kiongozi wa Wengi Bungeni Bw Aden
Duale.
Huku
akiandamana na wenyekiti wa kamati za Ulinzi na Mahusiano ya Nje na ile
ya Usalama wa Kitaifa, wabunge 15 wa mrengo wa Jubilee na wabunge Joseph
Nkaissery na Victor Munyaka kutoka Cord, Bw Duale alisema kuwa hoja
iliyo Bungeni kuhusu kesi zinazoendelea katika mahakama ya ICC hazina
athari zozote kwa kesi hizo.
Kiongozi huyo
wa Wengi alisema kuwa ataendeleza harakati zake za kushinikiza
kufanyiwa mageuzi kwa Sheria ya Uhalifu wa Kitaifa ambayo yanalenga
kuiondoa Kenya kutoka uanachama wa Mkataba wa Roma, kama
ilivyopendekezwa na Bunge mnamo Septemba 5 katika kikao cha maalum.
Wiki moja
Alisema kuwa amekuwa akiutayarisha mswada huo, na utakuwa tayari kuwasilishwa Bungeni katika muda wa wiki moja au mbili zijazo.
Alidokeza kuwa uamuzi uliopitishwa katika Kongamano la Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa vile vile haungeathiri kesi hizo.
Alisema kuwa idara ya sheria nchini ni thabiti na haitaruhusu taasisi yoyote kutoka nje kuiingilia Kenya.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!