ACHANA na mchecheto wa mashabiki, upepo umebadilika kwa viongozi, wachezaji mpaka makocha wa Simba na Yanga ambao wakiipigia hesabu za kiufundi mechi itakayowakutanisha Jumapili, wanasema ni denja sana.
Simba, ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara inapata kiburi kutokana na ufanisi wa wachezaji wake wa
kigeni pamoja na wazalendo wenye uzoefu.
Wachezaji hao wamekuwa wakichachafya katika kila
mechi ingawa benchi la ufundi limedai inapofika mechi ya watani wa jadi,
mambo huwa ni habari nyingine.
Yanga, ambayo haijafumua kwa kiasi kikubwa kikosi
kilichotwaa ubingwa msimu uliopita, imerudi kwenye fomu na ina ari kubwa
ya kutaka kuishusha Simba kileleni.
Tathimini ya mechi hiyo imekuwa ikizungumziwa zaidi kuanzia kwenye safu ya ulinzi, kiungo na washambuliaji.
Mabeki wa Yanga; Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ watakuwa na kazi moja tu ya kuzima makali ya Mrundi
Amisi Tambwe mwenye sifa ya kuliona lango kadiri atakavyo.
Tambwe ambaye Simba inamtumia akiwa straika wa
pili baada ya Betram Mwombeki, ana mbinu nyingi za kufunga tena katika
mazingira yoyote, iwe kwa kichwa au mguu.
Madhara yake yanakuwa makubwa zaidi anapocheza na
Mwombeki, straika mrefu mwenye nguvu. Mwombeki anatumiwa na kucheza
akiwa straika wa mwisho ili kuwachosha mabeki na hivyo kumpa urahisi
Tambwe kumaliza kazi.
Mwombeki atakuwa na kazi ya kuhakikisha
anacheza mipira yote ya juu na kumtengenezea Tambwe mipira ya mwisho na inayokufa ili amalizie jambo ambalo huenda likawatoa jasho Yondani na Cannavaro.
anacheza mipira yote ya juu na kumtengenezea Tambwe mipira ya mwisho na inayokufa ili amalizie jambo ambalo huenda likawatoa jasho Yondani na Cannavaro.
Hata hivyo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro, amewaambia mashabiki wake wasiwe na presha bali waende uwanja kifua mbele.
Wachezaji wengine wa kuogopwa katika kikosi cha
Simba ni mawinga; Haroun Chanongo na Ramadhani Singano ‘Messi’ ambao ni
damu changa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!