Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Kesi ya Barasa kutaka asipelekwe Hague kusikizwa Jumanne

Kesi ya Barasa kutaka asipelekwe Hague kusikizwa Jumanne

Written By Unknown on Monday, 14 October 2013 | Monday, October 14, 2013


KESI ya kuhamishwa kwa mwandishi habari Walter Opinyi Barasa hadi mjini Hague kujibu mashtaka ya kuwahonga mashahidi wasihudhurie kesi ya naibu wa rais William Ruto itasikizwa Oktoba 15.
Jaji George Odunga alisema Waziri wa Usalama Joseph ole Lenku alikuwa amemkabidhi Jaji Richard Mwongo barua aliyopokea kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ili amteue jaji atakayesikiza ombi hilo dhidi ya Bw Barasa.
“Ijapokuwa kila jaji yuko na mamlaka sawa na mwenzake, naelekeza kesi hii iwasilishwe mbele ya jaji anayesimamia Mahakama Kuu Jaji Richard Mwongo atoe mwelekeo na utaratibu wa kuisikiza,”akasema Jaji Odunga.
Mwandishi habari huyo anapinga ombi la ICC akamatwe na maafisa wa usalama nchini Kenya kisha wampeleke mjini Hague kujibu mashtaka.
Jaji Odunga alifahamishwa na wakili Wilfred Nderitu anayewakilisha wahanga wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 kwamba hakuna tofauti ya sheria za nchini humo na zile za ICC.
Haki
“Mshukiwa huyu atapata haki sawa kule ICC au nchini humo. Sheria za kimataifa zinazotumika ni sawa na zile zinazotumika nchini humo. Kenya ilitia sahihi  sheria zinazofungamanisha mataifa ya ulimwengu kupambana na uhalifu wa kimataifa,”akasema Bw Nderitu.
Wakili huyo alisema kuwa ni wajibu wa Mahakama kuu ya Kenya kuzingatia sheria na kuhakikisha kwamba haki imetekelezwa.
“Uamuzi wa kutiwa nguvuni kwa Bw Barasa ulitolewa na Jaji Okuno Takusa wa Mahakama ya ICC baada ya kiongozi wa mashtaka  Bi Fataou Bensouda kuwasilisha ombi,” akasema Bw Nderitu.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi