Wapinzani
nchini Guinea wanatarajia kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi
wa wabunge yaliyotangazwa hivi karibuni ambayo yaliyokipa ushindi
mkubwa chama tawala cha RPG kinachoongozwa na Rais wa nchi hiyo Alpha
Conde.
Msemaji wa muungano wa wapinzani Sydia Toure amesema kamwe
hawawezi kutambua matokeo ambayo hayawakilishi matakwa ya wananchi wa
Taifa hilo.
Naye mpinzani mkuu wa Rais Conde toka chama cha UDFG Cellou Dalein Diallo amesema wana uthibitisho wa kutosha juu ya udanganyifu uliofanyika katika zoezi la uchaguzi.
Hatua hiyo ya wapinzani imezusha hofu kuwa huenda machafuko
yakalikumba Taifa hilo lenye historia ya migogoro ya kisiasa na kijeshi
na umwagaji damu kwa waandamanaji.
Mkuu wa Umoja wa Taifa katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika, Said Djinnit ametoa wito kwa wapinzani kutafuta haki yao kwa kuzingatia misingi ya sheria na kuwa watulivu wakati wakisubiri maamuzi ya mahakama juu ya uhalali wa matokeo hayo.
Msemaji wa serikali Damantang Albert Camara amesema chama tawala kimeridhishwa na matokeo hayo ambayo yamehitimisha mchakato huo uliochukua muda mrefu kutamatika.
Hata hivyo waangalizi wa uchaguzi huo toka taasisi mbalimbali za kimataifa tarehe 9 ya mwezi huu walisema kulikuwa na dosari ngingi zinazoathiri uhalali wa matokeo ya uchaguzi huo.
Katika matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi siku ya ijumaa,
chama tawala cha RPG pamoja na washirika vyama wake katika uchaguzi huo
walipata jumla ya viti 70 kati ya viti 114 vya bunge zima, ambapo RPG
pekee ilipata viti 53 na washirika wake walipata viti 7.
Chama pinzani cha UFDG kinachoongozwa na Cellou Dalein Diallo kilipata viti 37 wakati chama cha Waziri Mkuu wa zamani nchini humo Sidya Toure cha UFR kilipata viti 10 na nafasi nyingine zilizosalia zimekwenda kwa vyama vidogo vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Matokeo hayo yametangazwa takribani majuma matatu baada ya zoezi la upigaji kura kufanyika, suala ambalo lilizidisha hofu kuwa huenda udanganyifu unafanyika ili kukipa ushindi chama tawala.
Naye mpinzani mkuu wa Rais Conde toka chama cha UDFG Cellou Dalein Diallo amesema wana uthibitisho wa kutosha juu ya udanganyifu uliofanyika katika zoezi la uchaguzi.
Hatua hiyo ya wapinzani imezusha hofu kuwa huenda machafuko
yakalikumba Taifa hilo lenye historia ya migogoro ya kisiasa na kijeshi
na umwagaji damu kwa waandamanaji.Mkuu wa Umoja wa Taifa katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika, Said Djinnit ametoa wito kwa wapinzani kutafuta haki yao kwa kuzingatia misingi ya sheria na kuwa watulivu wakati wakisubiri maamuzi ya mahakama juu ya uhalali wa matokeo hayo.
Msemaji wa serikali Damantang Albert Camara amesema chama tawala kimeridhishwa na matokeo hayo ambayo yamehitimisha mchakato huo uliochukua muda mrefu kutamatika.
Hata hivyo waangalizi wa uchaguzi huo toka taasisi mbalimbali za kimataifa tarehe 9 ya mwezi huu walisema kulikuwa na dosari ngingi zinazoathiri uhalali wa matokeo ya uchaguzi huo.
Katika matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi siku ya ijumaa,
chama tawala cha RPG pamoja na washirika vyama wake katika uchaguzi huo
walipata jumla ya viti 70 kati ya viti 114 vya bunge zima, ambapo RPG
pekee ilipata viti 53 na washirika wake walipata viti 7.Chama pinzani cha UFDG kinachoongozwa na Cellou Dalein Diallo kilipata viti 37 wakati chama cha Waziri Mkuu wa zamani nchini humo Sidya Toure cha UFR kilipata viti 10 na nafasi nyingine zilizosalia zimekwenda kwa vyama vidogo vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Matokeo hayo yametangazwa takribani majuma matatu baada ya zoezi la upigaji kura kufanyika, suala ambalo lilizidisha hofu kuwa huenda udanganyifu unafanyika ili kukipa ushindi chama tawala.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!