Hasheem Thabeet (Tanzania)
Ndio
mchezaji mrefu kuliko wote kwenye ligi ya NBA kwa sasa, majuzi wakati
timu yake ya Oklahoma City Thunder ikicheza na Charlotte Bobcats Hasheem
alicheza vizuri akiwa na point 13 alizofunga pamoja na kudaka Rebounds
10, huu utakua msimu wake wa pili akiwa na OKC.
Dieng
(23) amesajiliwa na Minnesota Timberwolves baada ya kufanya vizuri
akiwa na timu ya Louisville Cardinals inayoshiriki ligi ya vyuo vikuu
Marekani NCAA.
Ike ni mchezaji wa kiafrika ambae amewahi kucheza ligi ya NBA kwa muda mfupi kabla ya kwenda barani Asia alikochezea timu ya XINJIANG FLYING TIGERS, GUANGDONG SOUTHERN TIGERS na timu mbili za PUERTO RICO ambazo ni CAPITANES DE ARECIBOna LEONES DE PONCE ila kwa sasa anarejea kwa mara ya pili kwenye ligi ya NBA ambapo atachezea timu ya NEW YORK KNICKS.
Unaambiwa
moja ya majina makubwa kwenye mchakato wa kuchagua wachezaji wanaotoka
vyuoni mwaka 2011 lilikua jina la Bismack Biyombo ambae alichaguliwa na
timu ya SACRAMENTO KINGS na mwaka huu amesajiliwa na CHARLOTTE BOBCATS
ambako atakua akishindana kutafuta namba na Cody Zeller aliyejiunga na
timu hiyo msimu huu.
Carlos
Morais amesajiliwa kuichezea TORONTO RAPTORS msimu huu akiwa na uzoefu
wa kuiongoza Angola kwenye mashindano kadhaa ya kimataifa na amewahi
kucheza kwenye mashindano ya FIBA Afrika 2005 na 2007, mashindano ya
dunia mwaka 2006 pamoja na mashindano ya Olimpiki mwaka 2008.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!