ZAMBIA imetoa vibali vya
kukamatwa kwa wachezaji wake watatu waliokosa mechi ya kirafiki dhidi
ya Brazil mjini Beijing China mchezo ambao nchi hiyo ilifungwa kwa mabao
2-0. Klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ilisisitiza kuwa
wachezaji hao Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na
Nathan Sinkala
walijeruhiwa na kusababisha mgogoro kati ya Shirikisho la Soka la
Zambia-ZFF na serikali yake. Baada
ya wachezaji hao kufanyiwa uchunguzi jijini Lusaka, ZFF ikasisitiza
kuwa bado wanaweza kusafiri kwenda China kwa mechi hiyo, lakini klabu ya
Mazembe ambako wachezaji hao hucheza soka ya kulipwa ikawataka
kurejea. Hatua
hiyo ilisababisha serikali ya Zambia kuingilia kati kwa kuwapokonya
wachezaji hao pasi zao za usafiri ili kuwazuia kwenda kuchezea klabu yao
mjini Lubumbashi. Hata hivyo, wachezaji walifanikiwa kuvuka mpaka na wanaaminika kuwa nchini DRC. ZFF
limeandikia barua Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, na kulalamika kuwa
klabu ya Mazembe haikuwaruhusu wachezaji hao kushiriki majukumu yao ya
kimataifa.
Home »
michezo africa
» WACHEZAJI WATATU WA ZAMBIA HAWAJUI WALIPO AKIWEMO STOPILA SUNZU
WACHEZAJI WATATU WA ZAMBIA HAWAJUI WALIPO AKIWEMO STOPILA SUNZU
Written By Unknown on Wednesday, 16 October 2013 | Wednesday, October 16, 2013
Labels:
michezo africa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!