KOCHA wa timu ya taifa
ya Croatia, Igor Stimac ameamua kujiuzulu baada ya timu yake kupoteza
mchezo wake wa mwisho wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa kufungwa
mabao 2-0 na Scotland. Croatia
imeambulia alama moja pekee katika mechi za nne za kundi A na kuwaacha
katika nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Ubelgiji huku wakikabiliwa
na kibarua cha kucheza mechi za mtoano za mikondo miwili kwa ajili ya
kutafuta tiketi ya kwenda Brazil mwakani. Stimac alichukua mikondo ya kuinoa nchi hiyo mwaka jana akichukua mikoba ya Slaven Bilic. Akihojiwa
na Sky Sport mara baada ya mechi hiyo Stimac alisikitishwa na kipigo
hicho na kuomba kujiuzulu kwasababu ya matokeo mabovu ambayo kikosi
chake imepata katika mechi a karibuni.
. |
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!