Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » EL SHAABAB YAZIDI KUONGEZA MBINU ZA VITISHO BAADA YA UVAMIZI WA MAREKANI

EL SHAABAB YAZIDI KUONGEZA MBINU ZA VITISHO BAADA YA UVAMIZI WA MAREKANI

Written By Unknown on Wednesday, 16 October 2013 | Wednesday, October 16, 2013


Al-Shabaab imeongeza unyanyasaji wake kwa raia katika mji wa pwani wa Somalia wa Barawe kufuatia jaribio la kumkamata kiongozi mwandamizi wa al-Shabaab kulikofanywa na wanajeshi wa Marekani wa Navy SEALs mapema mwezi huu. 
Kila siku asubuhi tangu kutokea kwa operesheni ya Marekani, wapiganaji wa al-Shabaab wakiwa wamefunika nyuso zao, wameingia katika maduka na majumba ya wilaya hiyo na kuwanyanyasa watu, kukiwa na taarifa kwamba zaidi wa wanamgambo wa ziada 200 wamefika ili kuongeza nguvu mjini hapo.
"Hii sio hali rahisi, Tangu makomandoo wa Marekani walipofanya shambulio katika mji wa ufukweni wa Barawe, ambako nilisikia kulikuwa na wapiganaji wa al-Shabaab na maafisa wao waandamizi, matatizo mengi tunayokabiliana nau¡yo yameongezeka," alisema Asha Mumin, mwenye umri wa miaka 35 na mama wa watoto wanne anayeishi katika mji huo.
Mumin alivyambia vyombo vya habari kwamba wapiganaji pia wamewaamrisha watu kukabidhi simu zao za mikononi kwa ajili ya uchunguzi.
Katika saa za mapema siku ya tarehe 5 Oktoba, kikundi cha hali ya juu cha makomando wa Marekani walikuja ufukweni katika jaribio la kumkamata Abdulkadir Mohamed Abdulkadir "Ikrima", Mkenya mwenye asili ya Kisomali na anayedaiwa kuwa kamanda wa wapiganaji wa kigeni wa al-Shabaab. Misheni hiyo ilizimwa wakati makomando walipokabiliana na vita vikali na kutathmini kwamba ingeweza kusababisha hasara kwa vifo vingi vya watu wasio na hatia.
Ikrima anasemekana kuhusika moja kwa moja na uzingiraji wa siku nne wa al-Shabaab katika jengo la maduka ya kibiashara la Westgate mjini Nairobi ambalo lilisababisha vifo vya angalau watu 67.
Siku mbili baada ya uvamizi huo, al-Shabaab waliwateka nyara wafanyabiashara vijana watano, ambao bado haijulikani waliko, alisema mzee wa kimila Ali Ahmed.
"Waliwachukua vijana watano wanaume kutoka mji wa Barawe kwa njia tofauti. Wawili kati yao walifumbwa macho na kuchukuliwa kutoka kwa jumbani kwao na watu waliokuwa na silaha pamoja na ngwa vitambaa machoni na kuchukuliwa kutoka magari [ya kivita] wakati watatu wengine walichukuliwa kutoka madukani kwao waliyokuwa wanayamiliki katika soko la Barawe," Ahmed aliiambia Sabahi. "Hakuna mtu anayethubutu kuwauliza al-Shabaab kwa nini waliwachukua vijana hao."
Ingawa al-Shabaab siku zote wamekuwa wakiwanyanyasa watu huko Barawe, hii imeongeza kiwango cha vitisho tangu operesheni ya Marekani, Ahmaed alisema.
"Sio tu wanawateka nyara na kuwadhuru raia na wamiliki [vijana] wa biashara] wa Barawe, pia waliwateka nyara vijana watatu ambao walikuwa wapiganaji wao wenyewe kwa kuwashutumu kwa kuongoza operesheni ya Marekani huko Barawe [kwa sababu] wa matumizi yao makubwa ya intaneti", alisema.

Raia waomba serikali kuingilia kati

Watu wanakimbia kutoka soko la eneo hilo na wafanya biashara wanafunga maduka yao kila mara kunapozuka maneno kuwa wanamgambo wanakaribia, alisema Maryan Yusuf, mwenye umri wa miaka 38, na mmiliki wa duka la nguo sokoni hapo.
"Wakati wanachama waliopotoshwa wa al-Shabaab wanapokuja sokoni wakiwa wamefunika nyuso zao, wanawatisha watu bila sababu kwa kuwalazimisha waoneshwe wale wanaofanya kazi na makafiri," aliiambia Sabahi, "Hatujui chochote kuhusu hilo. Baadhi ya watu wanajaribu kujadiliana nao na jawabu wanayoipata ni kufungwa macho na kuchukuliwa."
Alisema alikuwa haelewi kwa nini wanamgambo wanamshuku kila mtu anayefanya kazi sokoni hapo kwa kushirikiana.
"Wanasababisha dhiki kubwa kwa sababu wanatulazimisha kutoa taarifa au kuwasaidia kuwasaka watu wanaowaelezea kuwa ni wajasusi miongoni mwa wafanyabiashara [wasio na hatia] ambao wanafanya kazi zao tu," Yusuf alisema.
"Ni wazi kwamba huku ni kutia chumvi kwa upande wa al-Shabaab wakati wanapojaribu kutoa sababu kwa matatizo wanayowasababishia watu wa Barawe, ambao tayari wanaishi katika hali ngumu za maisha ambazo zimesababishwa na wao kwa miaka mingi sasa," alisema.
"Ninatoa wito kwa serikali ya Somalia kuja na kutuokoa kutoka kwa al-Shabaab haraka inavyowezekana."
Kwa dhamira hiyo, Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Abdihakim Haji Mohamud Fiqi alisema wiki iliyopita kwamba vikosi vya kijeshi karibuni vitaanza operesheni za kuikomboa Barawe kutoka kwa al-Shabaab.
"Tuna nia na mpango wa kuwakomboa karibuni," alisema. "Na kama unavyojua, kwa kweli, al-Shabaab, popote tunapowashambulia, wao hawapigani, hawalindi, hujiokoa tu na kukimbia."
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi