Wakfu wa Mo Ibrahim umaemua kutokutoa tunzo yake ya juu kwa Mafanikio ya Uongozi Barani Afrika mwaka huu, ukitaja kukosekana na wagombea wenye hadhi, ilitangaza Kamati ya Tunzo hiyo siku ya Jumatatu (tarehe 14 Oktoba).
"Tuzo hii huwaenzi wakuu wa zamani wa nchi au serikali ambao wakati wa utawala wao wamefanya vyema sana katika kuziongoza nchi zao, na kwa kufanya hivyo wakawa na kigezo bora kwa kizazi kijacho," alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hiyo, Salim Ahmed Salim, ambaye pia ni katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Afrika na waziri mkuu wa zamani wa Tanzania.
Akitangaza matokeo ya Faharasa ya Ibarhim ya Utawala Bora Barani Afrika (IIAG) jijini London, Mo Ibrahim, mwenyekiti wa wakfu huo, alisema hakuna hata mmoja aliyetimiza vigezo vya tuzo hiyo ya juu, yenye thamani ya dola milioni 5 kwa miaka 10 na dola 200,000 kila mwaka maishani mwake.
"Tukisema tutakuwa na tuzo kwa uongozi uliotukuka, lazima tubakie kwenye hilo hilo. Hatutarudi nyuma. Hatusemi kwamba kila mwaka lazima tupate mtu," alisema Ibrahim.
Miongoni mwa washindi waliowahi kupata Tuzo ya Ibrahim ni Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji (mwaka 2007), Rais Festus Mogae wa Botswana (mwaka 2008), Rais Pedro Pires wa Cape Verde (mwaka 2011) na Rais Nelson Mandela wa Afrika ya Kusini (Heshima).
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!