Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Watu 20 wapoteza maisha wakiwemo watoto 15 baada ya boti waliyokuwemo kupasuka kwenye mto Niger

Watu 20 wapoteza maisha wakiwemo watoto 15 baada ya boti waliyokuwemo kupasuka kwenye mto Niger

Written By Unknown on Monday, 14 October 2013 | Monday, October 14, 2013

Boti ya Mali ikizama baada ya kupasuka
Boti ya Mali ikizama baada ya kupasuka
Watu Ishirini wamefariki dunia, wakiwemo watoto 15 , baada ya boti waliyokuwemo kupasuka usiku wa kuamkia leo kwenye mto Niger karibu na mji wa Mopti nchini Mali maafisa wamesema na kuongeza kuwa watu 23 hawajulikani walipo na wengine 120 wamenusurika.

Kamanda Dramane Diallo, kutoka timu ya huduma ya uokozi ameiambia AFP kuwa chanzo cha kupasuka kwa boti hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea.
Afisa mwandamizi wa serikali kamanda Naman Keita, amethibitisha idadi ya watu 20 kupoteza maisha na kuongeza kuwa watoto 15 ni miongoni mwa waliopoteza maisha ambapo zoezi la kutafuta manusura lilisitishwa usiku huo na litaanza tena leo asubuhi.
Kamanda Dramane pia amesema boti hiyo ilijazwa na mizigo kupita kiasi jamboa ambalo huenda likawa miongoni mwa sababu za kupasuka kwa boti hiyo.
Dramane ameongrza kuwa shughuli za uokozi za kikosi cha Mali zimefanyika kwa ushirikiano na wakazi wa mji wa Koubi pamoja na boti zingine zilizokuwa zikipita.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi