KIUNGO fundi wa Barcelona, Andres Iniesta, amekiri kutokuwa kwenye ubora wake na jambo hilo linamfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefanyiwa mabadiliko mengi kuliko yeyote kwenye La Liga msimu huu.
La Liga kumeibuka mjadala wa kukosoa viwango vya
ubora wa nyota watatu mahiri wa Barcelona; Iniesta, Xavi na Lionel Messi
ambao wanaonekana hawapo kwenye viwango vyao vilivyozoeleka.
Wakati hilo likiendelea kujadiliwa. Iniesta amejikuta akibaki kuwa mwathirika mkubwa wa kocha mpya, Tata Martino,
aliyekuja na mtindo wake wa kukibadili kikosi na kutaka wachezaji wake
wote wacheze huku Mhispaniola huyo akitumika si tena kama kiungo wa
kati.
Staa huyo amefanyiwa mabadiliko mengi kwenye
kikosi na hakika jambo hilo limeshaanza kumkwaza. Jumatano iliyopita
wakati mwamuzi wa akiba alipoonyesha bango kufanya mabadiliko
lililoonyesha namba yake, alionyesha ishara ambayo ilibainisha wazi
kuchukia kutolewa.
Kwenye mechi 18 ilizocheza Barcelona msimu huu,
Iniesta amecheza zote, lakini ni sita tu alizocheza kwa dakika 90, huku
saba akitolewa na tano akiingia kutokea benchi.
Kwenye mechi za hivi karibuni hakumaliza zote na
tayari hilo limewatia wasiwasi mashabiki wa Barcelona kwamba linaweza
kuathiri mpango wa kuongeza mkataba wa kubaki Nou Camp.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!