MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al-Ahly ya Misri jana Jumapili walifanikiwa kulitetea taji hilo baada ya kuichapa Orlando Pirates ya Afrika Kusini mabao 2-0 mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Arab Contractors, Cairo.
Mohammed Aboutrika aliipatia Ahly bao la kwanza
dakika ya 54 akiitumia vizuri pasi ya Abdullah Said ambaye mpira
alioupiga ulimbabatiza Gcaba kabla ya kumkuta mfungaji.
Kuingia kwa bao hilo kuliongeza ushindani kwa timu zote lakini ni juhudi za Ahly zilizozaa bao dakika ya 78 mfungaji akiwa ni Ahmed Abdul Zaher aliyeinasa pasi ya Ahmed Fathy.
Kuingia kwa bao hilo kuliongeza ushindani kwa timu zote lakini ni juhudi za Ahly zilizozaa bao dakika ya 78 mfungaji akiwa ni Ahmed Abdul Zaher aliyeinasa pasi ya Ahmed Fathy.
Pirates
ndio walioanza kwa kasi mechi hiyo, dakika ya tatu tu walifanya
shambulizi, Segolela alifumua shuti lakini mpira huo uliokolewa kiulaini
na kipa wa Ahly, Ekramy.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!