MKALI wa mabao wa Simba, Tambwe Amissi amewatamkia maneno ya maudhi mastraika wenzake wanaomfuatia kwenye safu ya ufungaji bora na kuwaambia: “Si mnaona, niliwaambia hamniwezi.”
Tambwe amerudi nchini kwa mapumziko mapema
kwa sababu anamuwahi mwanaye Flori ambaye ni mgonjwa na kwa sasa ndiye
kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 10.
Anayemfuatia ni Elius Maguli wa Ruvu Shooting ambaye ana mabao tisa wakati Hamis Kiiza raia wa Uganda wa Yanga ana manane sawa na Juma Luizio wa Mtibwa Sugar.
Akizungumza na vyo,bo vya Habari vya Tanzania,Tambwe alisema: “Kama
ninavyosema, mimi ni kama askari jeshi, ninapoingia vitani, napambana
hadi mwisho. Hatukufikia malengo ya kuongoza ligi, siumii sana kwani
tukirudi mzunguko wa pili tutakuwa vizuri”
“Narudi nyumbani kutuliza akili ili kujipanga upya, ”alisema.
Tambwe amesema hatawasahau mabeki wa Ruvu Shooting waliomchezea kindava huku akidai walimpiga mpaka ngumi. “Nakumbuka wale
mabeki wa kati wa ile timu ya jeshi inaitwa Ruvu, wale ni wakorofi
kuliko mabeki wote niliocheza nao katika ligi, wanatumia nguvu kupita
kiasi huku wakinitoa mchezoni kwa maneno ya kejeli na kama ningekuwa
legelege nisingeweza kucheza mbele yao,” alisema Tambwe.
Mabeki wa kati wa Ruvu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaozungumziwa na Tambwe ni Shaban Sunza ‘Chogo’ na George Michael ambao walikuwa wakipambana vilivyo na mshambuliaji huyo sambamba na Betram Mwombeki. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!