KOCHA wa timu ya AC Milan, Massimiliano Allegri amesisitiza kuwa Mario Balotelli alihitajika kuanzia katika benchi la wachezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Barcelona kwa manufaa ya timu na mshambuliaji huyo.
Balotelli
aliingizwa kama mchezaji wa akiba lakini alishindwa kubadili matokeo
baada ya Milan kulala kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Lionel Messi na moja
la Sergio Busquets.
Allegri
amesema Robinho alistahili kuanza katika mchezo huo badala ya Balotelli
ambaye anaamini kuwa bado hajakuwa fiti kutokana na majeraha yaliyokuwa
yakimsumbua.
Kocha
huyo aliendelea kudai kuwa Balotelli aliumia akiwa katika majukumu ya
kimataifa hivyo hakuona haja ya kumharakisha kumuingiza. Milan
inashika nafasi ya pili katika kundi H lakini wamekuwa wakifanya vibaya
katika Serie A na kujikuta wakiwa katika nafasi ya 11.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!