Timu ya soka ya Nigeria imenyakua kombe la dunia la michuano
ya soka kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17 (U-17)
iliyopigwa katika dimba la Mohammad Bin Zayeb huko falme za kiarabu.
Vijana hao wameandika historia ya pekee baada ya kupachika mabao 3-0
dhidi ya Mexico katika fainali za siku ya ijumaa.
Bao la kwanza lilipachikwa katika dakika ya 9 ambapo Mexico ilijifunga yenyewe kupitia kwa mchezaji wake Eric Aguirre.
Katika nusu ya pili ya mchezo huo Nigeria iliongeza mabao mawili kupitia Kelechi Iheanacho na Musa Mohammed.
Nigeria ilitwaa kombe hilo katika miaka ya 1985, 1993, 2007 na ushindi wa sasa unaipa historia ya pekee ya kuwa Taifa pekee duniani lililotwaa ubingwa huo kwa mara nne.
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Bletter ni miongoni mwa vigogo wa soka waliofika Abu Dhabi kushuhudia mtanange huo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!