Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » IWAPO MKUTANO WA JUMUIYA YA MADOLA UTAFANYIKA NCHINI SRI LANKA NA SISI HATUTOUHUDHURIA:Mauritania

IWAPO MKUTANO WA JUMUIYA YA MADOLA UTAFANYIKA NCHINI SRI LANKA NA SISI HATUTOUHUDHURIA:Mauritania

Written By Unknown on Wednesday, 13 November 2013 | Wednesday, November 13, 2013

Waziri mkuu wa Mauritius amekuwa kiongozi mwingine wa dunia kutangaza kususia mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kufanyika nchini Sri Lanka kwa kile nchi hiyo inadai haina rekodi nzuri ya kuheshimu haki za binadamu.

Mauritius inaungana na nchi za India na Canada ambazo tayari zimeshatangaza kutotuma mawaziri wake kuhudhuria mkutano huo kwa kile nchi hizo inadai kuwa Sri Lanka si muumini mzuri wa kuheshimu haki za binadamu hasa mara baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2009.
Sri Lanka inatuhumiwa na Jumuiya ya kimatiafa kwa wanajeshi wake kukithiri kwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kushiriki mauaji ya watu wa jamii ya Tamil na maelfu ya raia wasio na hatia wakati wa vita dhidi ya waasi wa kundi la Tamil Tiger.
Akihutubia bunge la nchini mwake, waziri mkuu wa Mauritius, Navin Chandra Ramgoolam amesema hatua inayochukua nchi yake ni ya kidemokrasia na kama taifa huru, linao uhuru wa kuamua mambo yake na jambo la kwanza ni kwakutohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola uliopangwa kufanyika nchini Sri Lanka.
Waziri Navin ameongeza kuwa nchi yake ambayo itaandaa mkutano ujao wa Jumuiya ya Madola mwaka 2015 inaamini kuwa suala la nchi wanachama kuheshimu haki za binadamu ni jambo la msingi na lakwanza kuzingatia kabla ya kuruhusu mkutano huu muhimu kufanyika nchini mwako.
Serikali ya Mauritius imesema imechukua hatua hii baada ya kufuatilia kwa ukaribu hatua zinazochukuliwa na nchi ya Sri Lanka hasa linapokuja suala la haki za binadamu na kubaini kuwa nchi hiyo mara kwa mara imekuwa ikikiuka mkataba wa kimataifa unaotambua haki za binadamu.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mauritius kutohudhuria mkutano wa nchi wanachama za Jumuiya ya Madola toka ijipatie uhuru wake mwaka 1968 na badala yake itawakilishwa na waziri wake wa mambo ya kigeni kwenye mkutano mwingine mjini Colombo.
India pia imesema itatuma mwakilishi wake na sio waziri mkuu huku nchi ya Canada yenyewe ikitia ngumu msimamo wake na kudai kuwa haitatuma hata mwakilishi kwenye mkutano huu.
Hii ni mara ya kwanza ka taifa zaidi ya moja kususia kuhudhuria mkutano wa nchi wanachama za Jumuiya ya Madola kwa madai nchi mwandaaji imekuwa na dosari nyingi za kutoheshimu haki za binaadamu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi