MWIGIZAJI wa kike wa filamu mwenye jina kubwa Bongo Wema Sepetu ‘Madam’
hivi karibuni alimpoteza baba yake mzazi aliyefariki katika Hospitali
ya TMJ kufuatia msiba huo Wema alifunguka kwa kudai kuwa baba yake
kilikuwa ni kiungo muhimu sana katika harakati zake za urembo na sanaa
kwa ujumla kwani baba yake alimuunga mkono katika kufanikisha ndoto
zake.
“Nimepoteza
mtu muhimu sana katika maisha yangu baba alikuwa akinisupport katika
sanaa kwani hata awali nilipotaka kuingia katika mambo ya ulimbwende
baba yangu aliniunga mkono, kulingana na nafasi yake kwa mzazi mwingine
isingekuwa rahisi kunikubalia kuingia katika mashindano ya umiss,”anasema Wema.
Wema
anasema hadi dakika za mwisho kabla ya baba yake kufariki alikuwa
akimwita Miss world, hata alipoingia katika sanaa ya uigizaji wa filamu
bado mzazi wake huyo alimuunga mkono jambo ambalo kwake lilikuwa ni
faraja na kujivua kuwa na mzazi anayetambua umuhimu wa kipaji cha
mwanaye.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!