KIPA namba moja wa Manchester City, Joe Hart, ataendelea kuonja makali ya kocha Manuel Pellegrini baada ya kuachwa benchi tena katika kikosi cha kwanza kilicho cheza dhidi ya CSKA Jumanne iliyo pita.
Hart
alifungwa bao la kizembe la Fernando Torres wiki iliyopita katika
pambano dhidi ya Chelsea na alikaa benchi wakati City ikiiadhibu Norwich City mabao 7-0 Jumamosi huku Pellegrini akiamua kumtumia kipa wa akiba, Costel Pantilimon.
Sasa imebainika kwamba Pantilimon ambaye ni kipa wa Romania, ataendelea kukaa katika lango la Manchester City, huku Hart ambaye ni kipa namba moja wa England akisugua benchi.
Hata hivyo, kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson, ametamka kwamba ataendelea kuwa na imani na kipa huyo katika kikosi chake cha England, licha ya kutupwa nje na Pellegrini.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!