Msanii aliyejipatia umaarufu sana kwa kuigiza kama tapeli ndani ya Bongo Dar es Salaam ‘Dude’, ameonesha kutoelewa kile kinachofanywa na wasanii wenzie wa Bongo Movie wa sasa katika kuhakikisha wanaipeperusha bendera ya nchi yao katika anga za kimataifa.
Dude ameeleza kuwa marehemu Steven Kanumba ndiye muigizaji pekee wa Bongo ambae aliitumia vyema fursa yake katika kuitangaza Tanzania kimataifa.
“Mimi nadhani ni msanii mmoja, hayati Steve Charles Kanumba ambaye alikuwa akitumia fursa yake vizuri kujitangaza na kutangaza soko la filamu nchini humu. Lakini kwa sasa hakuna kitu chochote kinachoendelea kwa wasanii wengine na ndio maana unakuta soko letu haliwezi kujulikana kimataifa.” Alisema
Kwa upande mwingine, Dude alitoa mtazamo wake kuhusu ujumuishwaji wa wasanii wachanga katika tasnia ya filamu nchini humo.
“Unajua tasnia ya filamu inazidi kukua ila bado kuzalisha wasanii wachanga wazuri (Upcoming Artist) ukiachana na wasanii wakongwe kama,JB, Vicent Kigosi (Ray), Wema Sepetu, Rich toka tuwaona enzi hizo kwenye tamthilia ya ‘Mambo Hayo’ lakini kwa sasa hakuna wasanii wazuri wachanga .”
Lakini pamoja na kuona hakuna muamko kwa wasanii wachanga, Dude anaona hali ni mbaya zaidi kwa wasanii wa kiume wanaochipukia kwa kulinganisha na wasanii wa kike.
“Afadhali hawa kidogo wakina Irene Uwoya,Rose Ndauka,Jackcline Wolper, kwa upande wa wanaume sijaona bado kama kuna wasanii wachanga wanaoweza kutufanya sisi wakongwe tuwe na hamu ya kusema kweli filamu yetu ina vipaji vipya na wasanii wakali.” Alisema Dude.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!