Ja rule alipotoka jela aliezea mengi mazuri aliyojifunza na kwamba alikuwa na muda wa kujiuliza na kujutia mabaya aliyoyafanya na kuyachukia pia.
Lakini hii ni tofauti kwa bingwa wa masumbwi wa zamani Mike ‘Iron’ Tyson ambaye amesema akiyakumbuka maisha yake ya jela anatamani hata ampasue mtu kichwa ili arudi tena jela!
Tyson ambae alifungwa miezi sita jela March 1992, kwa kosa la ubakaji ameelezea maisha yake ya jela kwenye kitabu anachoandika kuelezea maisha yake kwa ujumla alichokipa jina la ‘Undisputed Truth’.
Tofauti na kile kinachofikiriwa kuwa alikuwa anateseka sana alipokuwa jela, Tyson amefichua kuwa alikuwa anaishi maisha ya anasa kimtindo na kufanya mapenzi mara kwa mara na wanawake waliokuwa wanaenda kumtembelea.
Tyson ameandika kuwa alikuwa na tabia ya kuvunja amri ya sita na wanawake hao, lakini aliwahi pia kuvunja amri ya sita na mwanamke aliyekuwa anawafanyia counseling wafungwa ili kuwasaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Ameandika kuwa alimhonga mwanamke huyo kiasi cha $10,000 ili atengeneze paa la nyumba yake. Amesema alipokuwa ndani alikuwa amechoka kiasi cha kushindwa kwenda gym kufanya mazoezi hali iliyomshusha kiwango.
“Kuna wakati nakuwa kama naota kuhusu kumpasua mtu ubongo ili niweze kwenda jela maisha yangu yote, kufanyia kazi hiki kitabu kinanifanya niwaze kwamba maisha yangu yote yalikuwa utani.” Ameandika Tyson.
Kwenye ‘Undisputed Truth’, Tyson amefunguka mengi ikiwa ni pamoja na swala la kumdanganya mke wake kuwa ana ukimwi ili waachane, lakini hadi leo jamaa hana VVU wala UKIMWI.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!