Nchi ya
Tanzania imeahidi kuendelea kuwa mwanachama mwaminifu katika jumuiya ya
Afrika Mashariki EAC na kukanusha kuwa yenyewe imekuwa chanzo cha
kukwamisha maendeleo ya Jumuiya hiyo. Akilihutubia bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alhamisi hii mjini Dodoma, Rais wa nchi hiyo Jakaya
Mrisho Kikwete ameeleza kuchukizwa kwake na namna ambavyo baadhi ya
nchi wanachama wanataka kuharakisha shirikisho la Afrika Mashariki hata
kabla ya kufuata hatua muhimu za kuanzishwa kwake.
Kauli ya Rais Kikwete inatolewa wakati huu ambapo kumekuwa na
mgawanyiko wa dhahiri kwenye misimamo ya viongozi wa jumuiya kuhusu
masuala kadhaa ikiwemo miundo mbinu na utiwaji saini wa mikataba
inayohusisha jumuiya nzima.
Tanzania imeweka wazi kuwa haina mpango wa kujitoa EAC kwani haijaenda kunyume na mkataba wa jumuiya hiyo na imekuwa ikitumia gharama kubwa kuhakikisha jumuiya hiyo inaimarika.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, hata hivyo Tanzania na Burundi ndio zimeonekana kutengwa katika vikao vya hivi karibuni.
Kenya, Uganda na Rwanda zimeshafanya vikao vitatu Mombasa Kenya, Kampala Uganda na Kigali Rwanda, na viongozi wa nchi hizo waliamua mambo nane ya msingi ambayo yanaonekana kudhihiridha wazi tofauti za misimamo ndani ya jumuiya.
Rais Kikwete alisema wazi kuwa nchi hizo zimekiuka Mkataba wa EAC katika mambo manne kati ya mambo nane waliyoyajadili katika vikao vyao walivyovifanya.
Nchi ya Tanzania imekuwa na msimamo wa kupinga kuharakisha uundwaji wa shirikisho, hatua ambayo Rais Kikwete anasema inapaswa kwenda sambamba hatua kwa hatua na wala si kukurupuka.
Tanzania inataka hatua zifuatwe kwa kuanza na uundwaji wa umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na baadaye lifuate shirikisho la kisiasa, ambalo litafikiwa baada ya kura ya maoni ya wananchi wa nchi wanachama.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!