Kila kukicha talent za wanamuziki wa Burundi zazidi kupanda juu nakukubaliwa na watu tafauti duniani,Burundi ni nchi mojawapo ya Afrika mashariki ambayo tasnia ya Muziki aithaminiwi hata kidogo nakuchukuliwa kama mambo ya kihuni hata ukiwa mtu ambae unaegemea tasnia hiyo huwa wanakuona tofauti nakukuthaminisha na muhuni.
Burundi inawanamuziki ambao tayari walishaunda shirika la muziki na kulishikilia shirika hilo kama Mzazi mkubwa.
Kutokana na umaskini na kutokuwa na soko ya kazi ya muziki wa Burundi lakini pako wanamuziki bado wanazidi kushikamana na kazi hii ya muziki na waendelezaji hususani vipindi vya kusapoti huu muziki vinazidi kupatikana.kuna wasanii ambao hawapewi thamani hapa nchini nakuchukuliwa kama ma mbumbu ila ule mwenye akili anajihusisha na zingine kazi zaidi ya huu muziki.
Mwanamuziki rapa kutoka kaskazini mwa mjii mkuu wa Bujumbura na mmiliki wa kampuni ya Golden Rec namzungumzia KOO-K amelishangaza taifa la Burundi na warundi baada ya Video yake ya I M BACK NOW aliyo pewa shavu na Mnigeria Slim mwenye maikazi yake SWEDEN kuonekana kwenye Televisheni ya NIGERIA ya NIGEZEE TV kutoka huko
ni jambo ambalo limewashangaza wengi hadi mtangazaji Mh ISMAIL NIYONKURU kumtafuta huyu Mwanamuziki kwenye EXCLUSIF INTERVIEW.
Huyu kijana alionekana kufurahishwa na kitendo kwanza cha mtangazaji Mh ISMAIL NIYONKURU nakuanza kumpongeza saana kwa kumpigia sim asubuhi Live kwenye kipindi ambacho ni kipindi cha watu maarufu sana nchini BURUNDI.
KOOK-K alionekana kuwa mwenye furaha sana nakusema alifurahi saana kuiona video hiyo inachezwa NIGERIA nchi ambayo imejaza vipaji lukuki lakini video yake imechezwa kwenye Tv hiyo,KOOK-K alizidi nakusema kuwa atazidi kufanya kazi kwa bidii ili azidishe hapa alipo fikia.
KOOK-K anamiliki kampuni yake yakutengeneza Muziki kampuni ambayo inajulikana kama GOLDEN ENTERTAINMENT ikiwa na studio ya audio na visual na kutengeneza picha na sasa inasimamia wasanii kadhaa chipukizi
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!