Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MAKUBWA YAMKUTA STAR WA BONGO MOVIE NA MMILIKI WA KAMPUNI RJ

MAKUBWA YAMKUTA STAR WA BONGO MOVIE NA MMILIKI WA KAMPUNI RJ

Written By Unknown on Friday, 8 November 2013 | Friday, November 08, 2013

Klabu ya Bongo Movie ambayo inaundwa na baadhi ya wasanii wakubwa wa filamu nchini TANZANIA imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilo asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Ray alaumiwa sana.

Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii kutoka klabu ya Bongo movies (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.

Wataka kumjadili

Habari za uhakika zinasema kwamba, wasanii waliotangaza kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga marufuku wasanii hao kutoshiriki msiba wa mzee Sepetu huku akijua wema wa binadamu unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.
“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati akisambaza zile meseji alisahau kuwa kuna siku Wema aliwahi kuwaalika wasanii wa kundi la Bongo Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa, mbona hawakugoma kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.

Visingizio vya wanafiki “Tupa Kule”
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia baadhi ya wasanii waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo walisema walishindwa kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi kwamba walipokea meseji ya katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao kuulizwa kwa nini hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako location wanarekodi!
Mazito!! Msiba wa baba wema wamuweka Ray matatani, adaiwa aliwazuia watu kwenda msibani. Mwenyewe afunguka haya “Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa mnaweza kushikwa na ubize wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki, walisingizia vile ili ionekane wana hudhuru,” alisema staa mwingine.

Ray afunguka

Baada ya hayo yote hapo tuliamua kumfuatilia kwa karibu sana mwigizaji vicent kigosi ili yujue kama madai haya ni ya kweli aua la na haya ndo baadhi ya mambo aliyoweza kuyasema Ray.
“Kawaida yangu huwa sitetemeshwi wala kuyumbishwa na maneno yamesemwa.mengi sana juu yangu lakini Mungu wa haki ananipigania….kweli nimeamini ukubwa ni jalala na nyota yangu ni kubeba mizigo ya watu. Mtasema sana Lakini Yangu Yananinyokea..." Alimaliza Ray.
Mmmh. Haya sasa mazito. Sisi yetu macho.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi