MSHAMBULIAJI wa Simba, Amiss Tambwe amesema yupo kwenye mazungumzo na moja ya klabu za nchini Saudi Arabia iliyoonyesha nia ya kumsajili.
Straika huyo ambaye anaongoza katika ufungaji wa mabao akiwa amepachika 10, alijiunga Simba mwanzoni mwa msimu huu na amekuwa hatari kwenye ufungaji kiasi kwamba mashabiki wa Simba wamekuwa wakifurahia uwepo wake.
Tambwe amesema kuwa upo uwezekano wa kuondoka kwenye mzunguko wa pili au msimu ujao kama watakubaliana.
“Uwezekano wa mimi kuendelea kubaki Simba msimu ujao ni mdogo, kuna klabu ya Saudi Arabia imeonyesha nia ya kunihitaji.
Timu hiyo imeanza kufanya mazungumzo na meneja wangu aliyepo nyumbani Burundi, sitaweza kuitaja jina kwa sasa timu hiyo.
“Hivyo, nimepanga nitumie muda huu wa mapumziko kushughulikia masuala yangu ya usajili, nitaondoka nchini kwenda Burundi kesho (leo),” alisema Tambwe.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!