Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KWENYE MIRATHI YA KANUMBA MI NAKWAMBIA PATACHIMBIKA KWELI...BABA KANUMBA

KWENYE MIRATHI YA KANUMBA MI NAKWAMBIA PATACHIMBIKA KWELI...BABA KANUMBA

Written By Unknown on Friday, 8 November 2013 | Friday, November 08, 2013

Baba Kanumba 2

Ni zaidi ya mwaka mmoja umepita toka kufariki kwa mwigizaji staa wa Tanzania Steven Kanumba, ambae aliacha kampuni ya kutengeneza filamu aliyokua akiimiliki pamoja na mali nyingine yakiwemo magari.
Baba mzazi wa Marehemu Mzee Kanumba anaeishi Shinyanga amesema ‘kwenye mirathi tumeshirikiana na Mama Kanumba ingawa Jaji kachanganya baada ya kuwekwa watoto ambao sio wangu… mimi na mama Kanumba ni sahihi ila watoto ambao sio wangu tumeandaa Mwanasheria kuwaondoa wasiohusika na tumbo langu vinginevyo na wa tumbo langu waingie kwenye mgao wa mirathi’

‘Watoto walioshirikishwa na sio wangu ni Seth Bosco ambae ni mtoto wa shemeji yangu mdogo wake mama Kanumba, Tina Mshumbuzi, Bella Kajumulo yani haya majina unayaona yako tofauti, hawa wawili nilikuta Mama Kanumba ameshazaa.. kwa hiyo hawawezi kuingia kwenye kurithi ndio maana nafatilia Mahakama itende haki na watoto wangu waingie mule vinginevyo aisee patachimbika’ – Baba Kanumba

Kwenye sentensi ya mwisho Baba Kanumba amesema ‘Kanumba hakua na mke wala mtoto hivyo hawezi kuingia mwingine pale, mirathi ni ya watu wawili mimi na Mama Kanumba tuliemleta duniani Kanumba, sijawasiliana bado na Mama Kanumba…. tutawasiliana Mahakamani’
Baba Kanumba ambae hakuweza kuhudhuria maziko Dar es salaam kutokana na kuumwa, anasema kwenye mazungumzo ya mwisho na Marehemu siku kadhaa kabla ya kufariki, alimwambia kuhusu pesa zaidi ya milioni 50 alizokua nazo benki pamoja na nyumba aliyokua ameianza ujenzi Dar es salaam.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi