Home »
news
» NDOWA YA THEA NA MIKE SANGU HAIKO SAWA
NDOWA YA THEA NA MIKE SANGU HAIKO SAWA
NDOA
ya mastaa wa filamu, Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ imevurugika
baada ya kutokea hali ya kuzinguana kwa wawili hao chanzo kikidaiwa ni
kukosekana uwaminifu.
|
Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao. |
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa,
kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake
anamzunguuka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu
Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti
ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato)
anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu
ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu
tulitokea kutoelewana na si mambo ya meseji wala wanawake, mimi sina
mambo hayo kabisa, siwezi kuongelea mambo mengi mpaka nitakapoenda
nyumbani kwa mke wangu lakini kilichotokea ni cha kawaida tu .”Thea
hakuweza kupatika kuzungumzia ishu hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!