Home »
news
» NATAKA NIMUONE DIAMOND AKIWA KWENYE FURAHA,NIKO TAYARI KUCHANGIA TUNDA NA MWENZANGU:Penny
NATAKA NIMUONE DIAMOND AKIWA KWENYE FURAHA,NIKO TAYARI KUCHANGIA TUNDA NA MWENZANGU:Penny
MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’,
ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye
atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.
|
Penny katika pozi na Wema. |
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One,
alisema maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari
kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye amerejesha uhusiano
wake wa kimapenzi na mwimbaji huyo mpenda vidosho.
|
Nasibu Abdul ‘Diamond’. |
“Ninampenda Diamond na sitaki kumpoteza. Nia yangu ni kumuona akiwa
na furaha. Kama Diamond anaona kuna msichana mwingine wa kutoka naye na
kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka
awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.
|
Wema Sepetu 'Madam 'na Peniela Mwingilwa ‘Penny’. |
Kumekuwa na habari zisizo shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha
uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii
zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko
Ughaibuni.
Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni
amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania
mwaka 2006
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!