Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry |
Marekani imekuwa ikisisitiza kuwa ni lazima nchi ya Iran
ishirikiane na jumuiya ya kimataifa katika kupata suluhu ya mzozo uliopo
kabla ya kuondolewa vikwazo na kwamba uwajibikaji kwa nchi ya Iran ndio
unaotakiwa kushuhdiwa kwasasa.
Mkutano huo unawakutanisha Maofisa wa serikali ya Iran na wawakilishi toka Marekani, Uingereza, China, Ufaransa, Urusi na Ujerumani.
Mataifa ya magharibi yamekuwa yakiishuku Iran kuwa inatafuta uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia kupitia mpango wake huo lakini Tehran imekuwa ikikanusha na kusema kuwa lengo lao ni matumizi salama pakee.
Wakati huo huo Wiziri ya mambo ya nje ya Ufaransa imethibitisha kuwa Waziri wake Laurent Fabius atahudhuria katika kikao cha ijumaa hii mjini Geneva.
Iran kwa upande wake ina matumaini huenda makubaliano yakafikiwa kupitia mkutano huo, ingawa imeweka wazi kuwa haitakubali kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium badala yake inaweza kutekeleza baadhi ya maswala yanayozungumziwa.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!