Kamanda wa kijeshi wa waasi wa M23, Sultani Makenga |
Tayari msimamo wa Uganda kuhusu kutotaka kukabidhi wapiganaji
wa kundi hilo kwa Serikali ya Kinshasa imezua maswali mengi, huku baadhi
wakihoji iweje nchi hiyo ikatae kuwakabidhi watuhumiwa wa mauaji
mashariki mwa DRC?
Sultani Makenga akiwa na wapiganaji wa M23 zaidi ya 1500 walijisalimisha kwa jeshi la Uganda UDF siku ya alhamisi baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya serikali ya Kinshasa FARDC yanayoungwa mkono na vikosi vya Umoja wa Mataifa.
Awali msemaji wa jeshi la serikali ya Uganda Paddy Ankunda alifahamisha kuwa wapiganaji hao walijisalimisha mikononi mwa jeshi lao pamoja na Sultani Makenga katika eneo la hifadhi ya wanyama ya pori ya Mgahinga kwenye mpaka wa Uganda na DRCongo.
Uganda imekuwa mpatanishi wa mgogoro baina ya serikali ya Kinsasa na waasi wa M23, lakini mpaka sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyosainiwa ili kusitisha mzozo wa Mashariki mwa DRC uliosababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Kujisalimisha kwa wapiganaji hao kunakuja wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa UN umeahidi kuendelea kuisaidia serikali ya DRC kuimarisha usalama wa mipaka yake baada ya kufanikiwa kusambaratisha ngome zote za waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa M23 wametajwa katika orodha ya watuhumiwa wa wahalifu wa kivita wakikabiliwa na tuhuma za kuhusika na vitendo vya ubakaji, mauaji, utesaji na ushirikiswaji wa watoto katika majeshi yao.
Tanzania ambayo ni miongoni mwa mataifa yaliyopeleka wanajeshi wake katika brigedi maalumu ya UN huko Mashariki mwa DRC imepongeza hatua ya majeshi hayo kufanikiwa kusambaratisha ngome za waasi wa M23.
Akihutubia bunge la Tanzania siku ya alhamisi mjini Dodoma, Rais Jakaya Kikwete aliahidi Taifa lake kuendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha amani inarejea katika eneo la Mashariki mwa DRCongo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!