STRAIKA aliyeikwepa Simba na kwenda SC Villa ya Uganda ili apate nafasi ya kucheza fainali za Chan huenda akabugi kama Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litashikilia msimamo wake.
Emmanuel Okwi aliuzwa na Simba kwa Etoile du Sahel
ya Tunisia kwa ada ya Dola 300,000 lakini Watunisia hao wakashindwa
kuwalipa Simba fedha za usajili wa mchezaji huyo kwa wakati.
Okwi naye aligoma kuichezea timu hiyo akidai
kutolipwa haki zake na ndipo Uganda ilipowaomba Fifa wamruhusu aichezee
Villa kwa miezi sita wakati suala lake likitatuliwa.
Uganda ilitumia ujanja huo ili kumtumia mchezaji
huyo kwenye fainali za Chan zitakazofanyika mwakani ambazo wachezaji
wanaoshiriki ni wale wa ligi za ndani.
Hata hivyo kuna kila dalili kwamba mpango huo unaelekea kugonga mwamba.
Mmoja wa viongozi wa Shirikisho la Soka la Uganda
(Fufa), aliyekuwa akifuatilia fainali za Chalenji alisema kwamba bado mambo ni magumu ingawa alidai hawajataka iwe
rasmi kwa umma.
Alisema kwamba wamekuwa wakiwasiliana na CAF
ambayo imekuwa ikiwaambia kwamba Okwi si mali yao na hawawezi kumtumia
katika fainali za Chan.
CAF imekuwa ikiwaeleza mchezaji huyo ni mali ya Etoile na kwamba Villa wameazimwa tu.
“Okwi wanasema bado ni mchezaji wa klabu ya nje ya
Uganda na mkataba upo, hivyo tukimpeleka Chan inaweza kutuletea
matatizo makubwa.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!