Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MYAKA 15 JELA NDIYO AMBAYO AMEKATIWA MWANASIASA MPIZANI WA RAIS PAUL KAGAME,BI INGABIRE UMUHOZA

MYAKA 15 JELA NDIYO AMBAYO AMEKATIWA MWANASIASA MPIZANI WA RAIS PAUL KAGAME,BI INGABIRE UMUHOZA

Written By Unknown on Saturday, 14 December 2013 | Saturday, December 14, 2013

Mahakama ya rufaa nchini Rwanda imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela
kiongozi wa upinzani nchini humo Victoire Ingabire Umuhoza anayekabiliwa na kosa la uhaini. Hukumu hiyo imetolewa baada ya mwanasiasa huyo kukata rufaaa kupinga kifungo cha miaka nane alichokuwa akikabiliwa nacho hapo kabla.

Mahakama imethibitisha tuhuma zinazomkabili mwanasiasa huyo ambao ni ugaidi, kukuza chuki baina ya Wanyarwanda na kuhusika na mauwaji ya halaiki dhidi ya wanyarwanda kutoka jamii ya watutsi yaliotokea mwaka 1994.
Awali Ingabire alihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kutenda makosa ya uhaini kutokana na kufadhili vikundi vya kigaidi pamoja na kushiriki kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu laki nane nchini humo huku wengi wao wakiwa ni Watutsi.
Ingabire ambaye ni mpinzani mkubwa wa Rais Paul Kagame, aliwekwa jela tangu mwezi Oktoba mwaka 2010 na ameendelea kusisitiza kutotenda makosa ambayo yameelekezwa kwake akidai kile kinachofanyika kinamsukumo wa kisiasa.
Ingabire ambaye ni Mhutu na Kiongozi wa Chama Cha FDU alirejea nchini Rwanda mwaka 2010 mnamo mwezi Januari baada ya kuishi uhamishoni nchini Uholanzi baada ya kutajwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi