KIUNGO Mwingereza wa Arsenal, Jack Wilshere, yupo kwenye hatari ya kukosa mechi dhidi ya Chelsea baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kuwaonyesha kidole cha kati mashabiki wa Manchester City Jumamosi iliyopita.
Kutokana na kitendo alichofanya katika kipigo cha mabao 6-3, Wilshere anaweza kufungiwa mechi moja.
Kinachosubiriwa ni ripoti ya mwamuzi, Martin Atkinson, kuhusu mechi hiyo, lakini hata kama refa huyo atashindwa kulijumuisha tukio hilo kwenye ripoti yake, Chama cha Soka cha England (FA) kinaweza kuchukua hatua za kinidhamu kwa kutumia picha za televisheni.
Straika Luis Suarez aliadhibiwa kukosa mechi moja mwaka 2011 baada ya kutenda tukio linalofanana na hilo. Alifanya dhidi ya mashabiki wa Fulham baada ya Liverpool kuchapwa bao 1-0 pale Craven Cottage.
Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema hakuliona tukio lililofanywa na Wilshere, lakini akasema: “Kama amefanya na akaadhibiwa, tutakubali matokeo.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!