RIYAMA amesema kuwa anachukizwa na vitendo vya kimapenzi vinavyoonyeshwa kwenye filamu nyingi za sasa, ikiwemo mabusu ya staili ya kulana denda.
Riyama alisema kuwa zamani walikuwa wanapigana mabusu mashavuni kama ishara ya mapenzi na kusameheana, lakini sasa wanakula denda kabisa.
“Vitendo hivi ni uchafu wa wazi kwenye jamii, hata kama kuna namna ambavyo wanafanya lakini bado kuna tatizo, mtazamaji ambaye ni mtoto, kijana, mzee haelewi hilo, yeye anajua wanapeana denda kitendo hiki sikipendi,” alisema.
Riyama aliwajia juu wale wote wanaopenda kuigiza uzungu uliopitiliza kwa kuwa imekuwa ikizua lawama miongoni mwa wadau wa filamu.
“Hii ni ajira yetu, ni heshima kwa familia zetu, bado tuna nafasi ya kuifanya iwe bora na ya kuheshimika kuliko kuiga vitu ambavyo vinafanya ionekane katika mtizamo usio wa kiungwana wakati waigizaji ni waungwana kama watu wengine lakini matendo ndiyo yanayotuangusha,”alisema.
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa filamu zinazoigizwa nchini Tanzania kuhusisha vitendo vya aina hiyo licha ya baadhi ya watu kulalamika.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!