Chelsea ilijikuta ikiduwazwa kwa bao la dakika za mwisho la Oussama Assaidi katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Britannia.
Andre Schurrle aliifungia Chelsea bao la kuongoza, lakini mabao ya Peter Crouch na Stephen Ireland yaliifanya Stoke kuongoza, kabla ya Schurrle kusawazisha.
Hata hivyo, Assaidi alikuwa mtu wa mwisho kuamua matokeo ya mchezo huo kwa kufunga bao muhimu lililoipa pointi zote tatu Stoke City.
“Sijisikii vizuri kusema kitu kuhusu mchezo ule. Kwa kifupi ni kwamba tumefungwa mabao yakiwa pungufu kwa bao moja ukilinganisha na wenzetu. Sitaki kuzungumzia kiwango cha mchezaji mmoja mmoja, lakini kwa jumla mabeki wametuangusha,” alisema Mourinho.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!