MECHI zote za Ligi Kuu England zilizofanyika wikiendi hii
zilisimama kwa dakika moja kama sehemu ya kuomboleza kifo cha aliyekuwa
Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Mandela alifariki Dunia juzi Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Ligi Kuu England ilionyesha heshima yake kwa
kiongozi huyo kabla ya mechi saba zilizochezwa juzi Jumamosi na mbili
za jana Jumapili na moja ya leo Jumatatu kwamba zitasimama kwa dakika moja
kabla ya kuanza kama sehemu ya maombolezo.
Wakati huohuo, staa wa England aliyeipa taji la
ubingwa wa Kombe la Dunia, Sir Bobby Charlton ametoa salamu za
rambirambi kutokana na kifo cha Mandela, ambaye alikuwa rafiki yake
baada ya kutoka gerezani mwaka 1990. Charlton alikuwa akikutana mara kwa
mara na Mandela wakati alipokuwa akimtembelea nchini Afrika Kusini.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!