Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SHIRIKA LA HUMAN RIGHTS WATCH LIMETIWA HOFU NA HALI MBAYA INAYOZIDI KUENDELEA NCHINI AFRIKA YA KATI

SHIRIKA LA HUMAN RIGHTS WATCH LIMETIWA HOFU NA HALI MBAYA INAYOZIDI KUENDELEA NCHINI AFRIKA YA KATI

Written By Unknown on Friday, 20 December 2013 | Friday, December 20, 2013

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu duniani la Human Right Watch nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano nchini humo na kwamba nchi hiyo itatumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe hivi karibuni.Shirika hilo pia kwenye taarifa yake limesema kuwa vitendo vya mauaji ya halaiki na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu vimetekelezwa nchini humo na pande zinazokinzana.
Hivi karibuni wapiganaji wa kikristo wanaomuunga mkono rais aliyepinduliwa madarakani Francois Bozize wamekuwa wakiendesha vitendo vya mauaji dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa Seleka ambao baadhi yao wamejitenga na rais Michel Djotodia.

Katika hatua nyingine nchi ya Rwanda imeungana na Umoja wa Afrika katika kutuma wanajeshi zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kuleta amani kwenye taifa hilo ambalo kwa majuma kadhaa hivi sasa limeshuhudia machafuko makubwa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda, Louise Mushikiwabo amethibitisha nchi yake kutuma wanajeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati huku akishindwa kuweka wazi idadi kamili ya wanajeshi ambao wamepelekwa nchini humo.
Hapo jana pia wanajeshi kutoka nchini Burundi waliwasili kwenye mji mkuu wa taifa hilo Bangui kuungana na wanajeshi wengine wa Umoja wa Afrika walioko nchini humo.
Mpaka sasa idadi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika walioko nchini humo watafikia elfu 6 kuungana na wanajeshi zaidi ya elfu moja na mia sita wa Ufaransa ambao tayari wako nchini humo kutoa usalama kwa raia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi