Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema muelekeo wa Marekani kuhusu Mapatano ya Nyuklia ya Geneva ya Novemba 24 kati ya Iran na kundi la 5+1 ni ukiukwaji wa wazi wa vipengee vya mkataba huo.
Ayatullah Amoli Larijani ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran na kuongeza kuwa, ‘vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Mkataba wa Geneva’. Amesema ni jambo la kusikitisha kuwa Wamarekani wametoa tafsiri ya ajabu kuhusu Mkataba wa Geneva na jambo hilo halikubaliki. Amesema muelekeo huo wa Washington ni jambo ambalo limepelekea wananchi wa Iran wakose kuwa na imani na Marekani na waitifaki wake.
Mapatano ya Geneva yalifikiwa kati ya Iran na nchi za 5+1 ambazo ni China, Ufaransa, Russia, Uingereza, Marekani pamoja na Ujerumani. Kwa mujibu wa mapatano hayo, nchi hizo sita zilitambua haki ya Iran ya kurutubisha madini ya urani ambayo hutumika kuzalisha nishati ya nyuklia. Iran ilitakiwa ipunguze kiwango cha urutubishaji urani, nazo nchi sita zilipaswa kupunguzwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kutoiwekea vikwazo vipya. Hata hivyo Marekani tayari imeshakiuka mkataba huo na kuiwekea Iran vikwazo vipya.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!