Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UN YAPATA HOFU KUHUSU MACHAFUKO NCHINI SOMALIA

UN YAPATA HOFU KUHUSU MACHAFUKO NCHINI SOMALIA

Written By Unknown on Thursday, 19 December 2013 | Thursday, December 19, 2013


Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay, ameelezea hofu yake kuhusu machafuko ya hivi karibuni nchini humo.
Bwana Kay amesema machafuko yaliyoibuka katika maeneo kadhaa ya Somalia huenda yakatishia mchakato wa kurejesha amani na utulivu, pamoja na haki za maelfu ya raia walioathirika.
Ghasia zimeripotiwa karibu na Johwat katikati mwa Shabelle, maeneo ya Beledweyne Hiraan na Shebelle Kusini.
Ripoti zinasema kuwa wanamgambo wanawafurusha wakulima na wanavijiji katika mashamba wanapopanda mimea. Machafuko hayo yameelezwa kusababisha vifo, majeraha, kuwalazimisha watu kuhama makwao na uharibifu wa mali na mimea mashambani. Wanaoathiriwa zaidi hutoka kwenye jamii au kaya zenye watu wachache zaidi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi