Meneja wa Mariah Carey, Jermaine Dupri ameliambia gazeti
la New York Post kuwa hakufanya kosa lolote kutumbuiza kwa ajili ya rais
wa Angola, José Eduardo dos Santos anayeshutumiwa kuwa dikteta.
Carey alishutumiwa na shirika la Human Rights Foundation kufuatia show yake hiyo kitu ambacho Jermaine anasema hakimuingii akilini.
"Rais wa Marekani alipiga picha na binti wa jamaa huyu na kumpongeza mtu huyu kwa kukaa miaka mingi ofisini,” alisema Dupri."Kama anaweza kushikana mabega na watu hawa kwanini Mariah Care anashutumiwa kuwa amefanya kitu kibaya?”
Carey alitumbuiza kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na shirika la Red Cross nchini Angola (Dec. 15). Japokuwa muimbaji huyo wa Beautiful alionekana akiwa na familia ya dos Santos, Dupri alikiri kutokuwa na uelewa wa mambo aliyoyafanya rais huyo.
Shirika la Red Cross nchini Angola linaongozwa na mtoto wa rais huyo Isabel dos Santos.
Kwenye show hiyo Mariah Carey alilipwa dola milioni 1 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.6.
Mwaka 2008, Mariah Carey pia alitumbuiza kwenye familia ya Muammar Gaddafi.
Carey alishutumiwa na shirika la Human Rights Foundation kufuatia show yake hiyo kitu ambacho Jermaine anasema hakimuingii akilini.
"Rais wa Marekani alipiga picha na binti wa jamaa huyu na kumpongeza mtu huyu kwa kukaa miaka mingi ofisini,” alisema Dupri."Kama anaweza kushikana mabega na watu hawa kwanini Mariah Care anashutumiwa kuwa amefanya kitu kibaya?”
Carey alitumbuiza kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na shirika la Red Cross nchini Angola (Dec. 15). Japokuwa muimbaji huyo wa Beautiful alionekana akiwa na familia ya dos Santos, Dupri alikiri kutokuwa na uelewa wa mambo aliyoyafanya rais huyo.
Isabel Dos Santos |
Kwenye show hiyo Mariah Carey alilipwa dola milioni 1 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.6.
Mwaka 2008, Mariah Carey pia alitumbuiza kwenye familia ya Muammar Gaddafi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!