Kuna fununu zimekithiri kuwa mshambuliaji nyota wa
kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, Tresor Mputu
ameikacha klabu yake ya TP Mazembe na kuhamia kwa mabingwa wa soka
nchini Angola timu ya Kabuscorp. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28
inasemekana kuwa eti alitangazwa mbele ya waandishi wa habari jijini Luanda kuwa amesaini
mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya euro milioni mbili ambao
utamuwezesha kukunja kitita cha euro 40,000 kwa mwezi.
Mashabiki wa
Mazembe wamekuwa wakipinga kuondoka kwa nyota huyo hatua ambayo
imepelekea uongozi wa Mazembe kutoa taarifa ya kuwa kuondoka kwake
hakutaathiri kiwango cha timu hiyo. Mputu ameitumikia Mazembe kwa miaka
10 akiisaidia timu hiyo kushinda taji la Klabu Bingwa barani Afrika
mwaka 2009 na 2010 pamoja na kuweka historia ya kufika fainali ya
michuano ya Klabu Bingwa Duniani ambapo walifungwa na Inter Milan kwa
mabao 3-0 mwaka 2010. Timu ya Kabuscorp ilitengeneza vichwa vya habari
Januari mwaka jana wakati walipomsajili mshambuliaji nyota wa zamani wa
Brazil Rivaldo aliyecheza soka nchini humo kwa msimu mmoja pekee.
Japo taarifa hizo zikiwa kama fununu kocha mmiliki wa club hiyo tajiri M.Katumbi amekanusha taarifa hizo nakusema sizakweli,fahamu kama Mputu yupo Angola mapumzikoni ya hizi siku kuu,mmiliki wa klabu hiyo aliongeza nakusema kuwa anashangazwa na hizo taarifa baada ya kuziona kwenye magazeti na mitandao tafauti.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!